City Farm Project

City Farm Project Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from City Farm Project, Urban Farm, Nzuguni Nanenane, Dodoma.

Ubunifu ukiwa kiini Cha utendaji wetu, tunakuwezesha kulitumia eneo dogo nyumbani kwako kujizalishia chakula (nyama/matunda/mboga) Huku ukiyafanya mazingira yako yenye mvuto zaidi.

Sungura.👉Mama mmoja, 👉watoto kumi 👉kwa wakati mmoja!Chanzo hakika Cha utoshelevu wa kitoweo Safi na salama.City Farm Pro...
07/06/2022

Sungura.
👉Mama mmoja,
👉watoto kumi
👉kwa wakati mmoja!
Chanzo hakika Cha utoshelevu wa kitoweo Safi na salama.
City Farm Project
Fruitfulness at every house.

Mgomba
07/05/2022

Mgomba

06/05/2022

Ubunifu ukiwa kiini Cha utendaji wetu, tunakuwezesha kulitumia eneo dogo nyumbani kwako kujizalishia

WARAKA WA KWANZA WA KIJASIRIAMALI WA SANGA KWA WAAJIRIWA(Nakala kwa wanaolia na waliopaniki kwa kukosa ajira)Ndugu waaji...
01/05/2022

WARAKA WA KWANZA WA KIJASIRIAMALI WA SANGA KWA WAAJIRIWA

(Nakala kwa wanaolia na waliopaniki kwa kukosa ajira)

Ndugu waajiriwa popote mlipo,
Ninawasalimu kwa salamu za bashasha.

Kwanza ninawapongeza kwa fursa mliyopata kuwemo miongoni mwa wateule wachache, waliopata "job". Ni haki yenu kuitwa wateule maana huku mtaani kuna mamilioni wanawatamania. Mimi sielewi nani ni nani huko, lakini nimethibitisha kwamba mpo wengi sana ambao woga, uzembe, kukariri na kukosa taarifa ndio vimepelekea muwe waajiriwa lakini "destinies" zenu ni katika kujiajiri na kuwa waajiri. Uwongo kweli?

Waraka wa leo hauna maneno magumu. Lakini nyaraka nne zingine zijazo hakika zitakuwa ngumu kwenu. Hadi mwisho wa nyaraka hizi, ikiwa uliajiriwa simply kwa kigezo kwamba unatafuta mtaji, ama uoga, ama kukosa taarifa, hakika utachana-chana hiyo "salary slip mentality", na kuelekea kunakokuhusu. Ila ninyi wengine ambao ni waajiriwa wa kudumu (hadi kustaafu) ninataka niwasaidie kitu pia.

TWENDE..

Ni kweli kwamba sio lazima kila mtu awe na fedha nyingi kwenye maisha lakini NI LAZIMA kila mtu awe na fedha za KUTOSHA katika maisha. Bila kuwa na fedha za kutosha, whether you are a mchungaji, daktari, ticha, mubunge, waziri or mulinzi wa getini, ukweli ni kwamba utakuwa na "frustrated" maisha no matter unajifariji kiasi gani!

Kuna watu mmevuviwa kuajiriwa kiasi kwamba ukigusia tu ujasiriamali "mnawaka" na kujitetea kuwa wote hatujaumbwa kuwa wajasiriamali. Utetezi huu una matege na mie ngoja niunyooshe kwa kukujulisha mambo sita ya kukusaidia:-

1. Binadamu wote (nasisitiza wote) tuliumbwa tuwe wajasiriamali isipokuwa sio wote tulioumbwa kujiajiri 100%. Ujasiriamali ni kitu cha kiuumbaji ndani ya kila mtu (yaani kipo tu), isipokuwa kujiajiri ni kitu cha KIMAAMUZI. K**a unabisha kasome Mwanzo 1 & 2

2. K**a ukiajiriwa na ikatokea unalipwa mshahara unaotosha unaweza "kugoma", kutojiongeza kiujasiriamali. Hata hivyo, mishahara mingi duniani pote imebuniwa kuhakikisha mwajiriwa anapata fedha isiyomtosha na mishahara yote hubuniwa kufanikisha mambo makubwa matatu: ili mwajiriwa a) aendelee kuwa mnyenyekevu kwa ajira yake b) aendelee kukumbuka kurudi kazini mwezi baada ya mwezi c) aamini kuwa hakuna maisha nje ya kuajiriwa. Kitakachokupa fedha za kutosha mara nyingi kitakuwa ni ujasiriamali unaoufanya nje ya mshahara boundaries

3. Duniani kote waajiriwa wote hulipwa asilimia 10 ama chini ya hiyo kwa wanachozalisha. Yaani ukiona unalipwa laki nane basi ujue unazalisha thamani ya zaidi ya milioni nane. Ukiona unalipwa milioni tano, ujue uwezo wako wa kiuzalishaji ni zaidi ya milioni hamsini. Hii ni kwamba k**a leo ukiamua kujiongezea kipato nje ya mshahara unaweza kuzalisha zaidi ya mshahara unaolipwa kila mwezi kwa sababu uwezo huo unao! Na pia ni kwamba k**a leo ukiamua kuacha ama ukaachishwa ajira utakuwa na maisha mazuri kiuchumi kushinda uliyonayo sasa. You know why? Unazalisha milioni nane wanakulipa lake nane, k**a ukiwa your own boss, ukizalisha milioni nane zote zinakuwa zako. You see?

4. Yesu Kristo alipofundisha sala ya baba yetu kuna kitu cha kiuchumi alikiweka sawa kisemacho, "...utupe leo mkate wetu/riziki zetu za kila siku". Hakusema riziki/mkate wa kila mwezi, bali wa kila siku. Hii ni kwamba design ya Mungu ni kwamba kila mtu awe na chanzo cha kipato cha kila siku. Kwa hiyo, k**a umeajiriwa na unapata riziki/mkate wa kila mwezi pekee, please make sure kwamba unafanya juu chini kutafuta kajisehemu ka kukupatia walau mkate wako wa kila siku unapoendelea na limkate la kila mwezi. Otherwise utakua una-abuse sala ya Baba Yetu.

5. Biblia inasema mtu mwenye hekima (yaani anaejielewa) huacha urithi wa mali kwa watoto wa watoto wake (It mean wajukuu). Kimsingi ajira nyingi hasa za "Kibongo-bongo", hazina jeuri hata ya kukupa uwezo wa kuwajengea watoto wako nyumba na mali zingine, seuze kuwafikia wajukuu? Infact, ajira nyingi ziko soo limited kiasi kwamba kufanikiwa kujenga nyumba yako ya maana ya kwako binafsi na maybe kumiliki magari mawili matatu ya maana ni muujiza wa hadhi ya kutangazwa kwenye TV. Can you imagine!

6. Ujasiriamali wa kuzalisha kipato ni suala lisilokwepeka kwako mwajiriwa. Usipoufanya sasa kwa hiari basi utakuja kuufanya kwa lazima utakapostaafu. Uchaguzi unabaki mikononi mwako, kuanza sasa ama kusubiri

SO WHAT?

Sisemi, sijasema na hutakaa unisikie nikisema kwamba kuajiriwa ni kubaya. Isipokuwa lengo la waraka huu ni kukufikirisha kiutofauti kuhusu ajira yako. Ili kwamba ujionee mwenyewe ya kwamba ukitaka kuishi maisha atleast yasiyo na stress ni lazima ujifunze na uamue kufanya kitu ama vitu vya kujiongezea kipato nje ya mshahara.

Kwa mkono wangu nimesaini na kuweka muhuri,

Kwanini matunda ni adimu kwako? Mche mmoja unakutosha kabisa.Muhimu iwe mbegu Bora!0674181033
29/04/2022

Kwanini matunda ni adimu kwako? Mche mmoja unakutosha kabisa.
Muhimu iwe mbegu Bora!
0674181033

JE NI KWELI NGURUWE WANALIPA?Hesabu tunazokokotoa hapa chini zinazingatia vipimo vya uzalishaji na majedwali yaliyomo kw...
26/04/2022

JE NI KWELI NGURUWE WANALIPA?

Hesabu tunazokokotoa hapa chini zinazingatia vipimo vya uzalishaji na majedwali yaliyomo kwenye kitabu chetu!!

>Nguruwe mmoja toka anapozaliwa mpaka kufikia uzito wa kilo 90 atachukua siku 206 ambazo ni karibia miezi saba.

>katika siku hizo zote atakula kilo 292 za chakula ukizingatia mchanganuo katika jedwali namba 3 wa kulisha.

>Jedwali namba 2 la vyakula, mchanganyiko namba 3 unaghalimu takribani Tsh. 51000 kwa kilo 100. Inamaana kilo 1 ya chakula ni Tsh. 510. Kwa iyo kilo 292Ă—510 = 148,920. Hii ni gharama ya kulisha nguruwe mmoja miezi 7.

>Matunzo na gharama nyingine zinakadiriwa kuwa Tsh. 200 kwa siku. Kwaiyo 200Ă—206 (siku zote) = 41,200 Tsh.

>Gharama za kumtunza nguruwe mmoja, yaani chakula na matumizi mengine itakuwa: 148,920+41,200= 190,120 Tsh.

>Kwa nguruwe wa kilo 90 tumesema kitabuni kwamba utapata nyama asilimia 65 hadi 80 (umeshatupa uchafu wote yaani kicha, miguu, utumbo n.k.) tuchukue kiwango cha chini, hivyo; 65%Ă—90kg= kilo 58.5 za nyama.

>Kilo ya nyama kadiria ni Tsh 5000. Hivyo 5000Ă—58.5= 292,500 Tsh.

>Faida ni sawa na mapato toa matumizi: 292,500 - 190,120= 102,380 Tsh.

>Tumesema katika kitabu kwamba nguruwe 1 atakupa watoto 14 kwa mwaka makadirio ya chini kabisa (tumeshatoa idadi ya watoto wanaoweza kufa katika ukuaji)

>kwa iyo 14Ă—102,380 =1,433,320 Tsh. Hii ni faida unayoipata kwa watoto wa nguruwe mzazi mmoja.

>Kumbuka hesabu hii inatoka kwa nguruwe mmoja, ukikokotoa kwa kundi la nguruwe unapata faida na “economies of scale” hivyo gharama zinaweza kupungua na faida kuongezeka.

>MUHIMU: Ni lazima utumie mchanganuo na vyakula tulivyoweka kwenye kitabu ili ufikie uzito huo kwa wakati tajwa.

Je ni kweli nguruwe wanalipa??
Kupata kitabu chetu, Tsh. 6000
0755 639 835JE NI KWELI NGURUWE WANALIPA?

Hesabu tunazokokotoa hapa chini zinazingatia vipimo vya uzalishaji na majedwali yaliyomo kwenye kitabu chetu!!

>Nguruwe mmoja toka anapozaliwa mpaka kufikia uzito wa kilo 90 atachukua siku 206 ambazo ni karibia miezi saba.

>katika siku hizo zote atakula kilo 292 za chakula ukizingatia mchanganuo katika jedwali namba 3 wa kulisha.

>Jedwali namba 2 la vyakula, mchanganyiko namba 3 unaghalimu takribani Tsh. 51000 kwa kilo 100. Inamaana kilo 1 ya chakula ni Tsh. 510. Kwa iyo kilo 292Ă—510 = 148,920. Hii ni gharama ya kulisha nguruwe mmoja miezi 7.

>Matunzo na gharama nyingine zinakadiriwa kuwa Tsh. 200 kwa siku. Kwaiyo 200Ă—206 (siku zote) = 41,200 Tsh.

>Gharama za kumtunza nguruwe mmoja, yaani chakula na matumizi mengine itakuwa: 148,920+41,200= 190,120 Tsh.

>Kwa nguruwe wa kilo 90 tumesema kitabuni kwamba utapata nyama asilimia 65 hadi 80 (umeshatupa uchafu wote yaani kicha, miguu, utumbo n.k.) tuchukue kiwango cha chini, hivyo; 65%Ă—90kg= kilo 58.5 za nyama.

>Kilo ya nyama kadiria ni Tsh 5000. Hivyo 5000Ă—58.5= 292,500 Tsh.

>Faida ni sawa na mapato toa matumizi: 292,500 - 190,120= 102,380 Tsh.

>Tumesema katika kitabu kwamba nguruwe 1 atakupa watoto 14 kwa mwaka makadirio ya chini kabisa (tumeshatoa idadi ya watoto wanaoweza kufa katika ukuaji)

>kwa iyo 14Ă—102,380 =1,433,320 Tsh. Hii ni faida unayoipata kwa watoto wa nguruwe mzazi mmoja.

>Kumbuka hesabu hii inatoka kwa nguruwe mmoja, ukikokotoa kwa kundi la nguruwe unapata faida na “economies of scale” hivyo gharama zinaweza kupungua na faida kuongezeka.

>MUHIMU: Ni muhimu utumie mchanganuo na vyakula tulivyoweka kwenye kitabu ili ufikie uzito huo kwa wakati tajwa.

Je ni kweli nguruwe wanalipa??
Kupata kitabu chetu, Tsh. 6000
0755 639 835

PAPAIMche mmoja K**a huu unaweza kutosheleza mahitaji yako ya papai nyumbani.Mambo ya kuzingati:👉Aina ya mche(mbegu)👉Maa...
13/04/2022

PAPAI
Mche mmoja K**a huu unaweza kutosheleza mahitaji yako ya papai nyumbani.
Mambo ya kuzingati:
👉Aina ya mche(mbegu)
👉Maandalizi ya shimo
👉Uchanganyaji wa mbolea.
Inawezekana ukachuma tunda hapohapo nyumbani kwako.
Karibu
CITY FARM PROJECT

11/04/2022

Address

Nzuguni Nanenane
Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when City Farm Project posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to City Farm Project:

Share

Category


Other Urban Farms in Dodoma

Show All