Ufugaji Digital -MAPS

Ufugaji Digital -MAPS Wataalamu wa sayansi ya wanyama na uzalishaji. Tunashauri na kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa na kibiashara, na uendeshaji wa miradi hiyo kwa faida.
(27)

Wakati mahitaji ya mazao ya mifugo yakiongezeka kwa kasi, gharama za ufugaji nazo zimekuwa zikipanda kwa kasi. Kwa wafugaji ni changamoto maana wanahitaji faida ili kukuza shughuli zao. tatizo kubwa ni ombwe la utaalamu sahihi badala yake wafugaji kuchangannywa na taarifa zisizokuwa na utaalamu wa kisayansi ndani yake. lengo la .digital ni kuziba ombwe hilo kwa kutoa elimu, ushauri, dondoo na kushirikishana uzoefu na wafugaji. UFUGAJI NI BIASHARA

Watoto kumi Mara moja! Waooh!!Shambani kwetu ni City Farm Project
08/06/2022

Watoto kumi Mara moja!
Waooh!!
Shambani kwetu ni City Farm Project

29/04/2022

Kwanini matunda ni adimu kwako? Mche mmoja unakutosha kabisa.
Muhimu iwe mbegu Bora!
0674181033

01/09/2020
Unastahili Miche Bora kabisa, nambie wewe unataka ipi?Utaletewa popote nchini.
14/02/2020

Unastahili Miche Bora kabisa, nambie wewe unataka ipi?
Utaletewa popote nchini.

10/02/2020

Karibu Miche ya matunda ya muda mfupi Aina zote.
👉Miche imepandikizwa (budding/grafting)
Dodoma na mikoa jirani.

04/11/2019

ARDHI HEKALI 10 ZINAUZWA JIJINI DODOMA. KWA MAHITAJI
0674181033

Sungura👉Hula majani na mchanganyiko mwingine want mabaki ya chakula nyumbani.👉Hawashambuliwi Sana na magonjwa.👉Huzaliana...
17/10/2019

Sungura
👉Hula majani na mchanganyiko mwingine want mabaki ya chakula nyumbani.
👉Hawashambuliwi Sana na magonjwa.
👉Huzaliana kwa Kasi.
Kwaiyo.
👉Gharama za ufugaji wake sio kubwa kulinganisha na mifugo mingine.
👉Idadi yake inaweza kuongezeka kwa Kasi na ivyo kuleta faida kwa mfugaji.

SassoKuku Safi kabisa wenye miezi mitatu Sasa.Wastani was uzito Ni 1.5 mpaka 2.5 Kg.Yapi majogoo mazuri ya mbegu na nyam...
26/05/2019

Sasso
Kuku Safi kabisa wenye miezi mitatu Sasa.
Wastani was uzito Ni 1.5 mpaka 2.5 Kg.
Yapi majogoo mazuri ya mbegu na nyama pia.
Wanna afya nzuri na chanjo zote.
Wapi Dodoma jiji.
Bei maelewano
Unaletewa kuanzia 10.
Kwa mahitaji
0674181033

01/04/2019
15/09/2018

Protini ni kirutubisho muhimu sana katika ujenzi wa mwili wa mnyama! lakini ndiyo vyakula vya gharama zaidi (mf. dagaa, mashudu n. k) Hivyo mfugaji akipata u...

07/07/2018

Chatara miezi 3
#12,000 unawapata. miezi miwili ijayo watakuwa wanataga vizuri.
Ni Dodoma jijini.

17/05/2018

Chotara wa mwezi mmoja na wiki mbili. Kwa ulishaji bora na matunzo makini!

AZOLLA Unajua jinsi ya kutengeneza Bustani ya Azolla nyumbani kwako?? ni rahisi tu, kwa nini uingie gharama kubwa za cha...
23/01/2018

AZOLLA
Unajua jinsi ya kutengeneza Bustani ya Azolla nyumbani kwako??
ni rahisi tu, kwa nini uingie gharama kubwa za chakula cha mifugo yako!!?
Video hii

Protini ni kirutubisho muhimu sana katika ujenzi wa mwili wa mnyama! lakini ndiyo vyakula vya gharama zaidi (mf. dagaa, mashudu n. k) Hivyo mfugaji akipata u...

  Fahamu namna ya kumhasi nguruwe! Mambo yote
23/01/2018


Fahamu namna ya kumhasi nguruwe!
Mambo yote

kuna faida nyingi za kuhasi nguruwe. moja ni kuepusha uzalianaji usio na mpangilio hasa kati ya nguruwe ndugu. je unajua kuhasi nguruwe? JIFUNZE

HABARI NJEMA DODOMAJe ufugaji wako unaufanyia Dodoma??Fursa za maendeleo ya sekta ya ufugaji pamoja na upatikanaji wa ma...
25/08/2017

HABARI NJEMA DODOMA

Je ufugaji wako unaufanyia Dodoma??
Fursa za maendeleo ya sekta ya ufugaji pamoja na upatikanaji wa masoko ya bidhaa zake zinaongezeka kwa kasi Dodoma.

Sasa unaweza kupata vitabu bora kabisa vya "Ufugaji bora na wa kibiashara wa kuku wa asili, bata na kanga" na "ufugaji wa nguruwe" hapa hapa Dodoma.

Unaweza pia kupata ushauri wa kitaalamu katika kuanzisha, kuendesha, ama kuboresha miradi ya ufugaji kibiashara.

Mawasiliano
0755639835/ 0689494521

Unasumbuka kufuga mifugo asili (kuku, bata na kanga) kwa ajili ya kukosa maarifa!!?? 👇Hii ni kwa ajili yako👇Kaa tayari, ...
09/07/2017

Unasumbuka kufuga mifugo asili (kuku, bata na kanga) kwa ajili ya kukosa maarifa!!??
👇Hii ni kwa ajili yako👇
Kaa tayari, ni hivi karibuni!

05/07/2017
Chanjo muhimu za kuku!! Ufugaji Digital -MAPS0755 639 835 0689 494 521 (watsapp)
01/06/2017

Chanjo muhimu za kuku!!
Ufugaji Digital -MAPS
0755 639 835
0689 494 521 (watsapp)

MCHANGANUO WA GHARAMA NA FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU WA MAYAITaarifa sahihi hupelekea maamuzi sahihi. Tumekuwa tukisisitiza...
28/05/2017

MCHANGANUO WA GHARAMA NA FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU WA MAYAI

Taarifa sahihi hupelekea maamuzi sahihi. Tumekuwa tukisisitiza kwamba ‘ufugaji ni biashara’ k**a biashara nyingine hivyo mipango na mikakati itokanayo na taarifa sahihi pekee ndiyo inayoweza kumletea mfugaji faida! Hebu tutazame kuku wa mayai…

🐓Kifaranga mwenye umri wa wiki 1 hadi 6 hula wastani wa gramu 35 kwa s**i ambayo ni sawa na kilo 1.5 katika wiki zote sita.
🐓Tetea mwenye umri wa wiki 7 hadi 17 hula wastani wa gramu 80 kwa siku, katika wiki hizi 10 atakula kilo 5.6.
🐓Kuku anayetaga, mwenye wiki 17 na kuendelea hula wastani wa gramu 120 kwa siku.
👉Gharama (wastani) za jumla za chakula bora (kwa fomula tulizonazo) ni 80000 Tsh kwa kilo 100.

Kwa hiyo:
👉Katika hatua ya kifaranga kuku atakula chakula cha 1200, na tetea atakula cha Tsh. 4480 na jumla katika hatua ya kifaranga na tetea atakula Tsh 5680.
👉Kuku anayetaga atakula Tsh. 96 kwa siku na katika miezi 6 (siku 180) ni sawa na Tsh. 17280.
🐓Hivyo, toka siku ya kwanza unapoanza kufuga kifaranga mpaka unapokamilisha mwaka; utamlisha chakula cha 22,960 Tsh.

🐔Katika mwaka (miezi 12) miezi 6 ya kwanza atakuwa hatua ya kifaranga na tetea (hatagi) na miezi 6 ya pili anakuwa anataga!
👉Hivyo hiyo miezi 6 atakayotaga ni sawa na siku 180, na kuku mzuri atataga kwa 80% ya siku hizo. Hivyo yatakuwa mayai 144. K**a ukiyauza kwa tsh. 250 utapata Tsh. 36000.

Lakini.
💲Gharama za chakula katika ufugaji wa kuku ni 70% ya gharama zote (wastani).
👉Kwa iyo k**a 22,960 ni asilimia 70% ya gharama zote basi asilimia 100 ya gharama zote ni 32,800 kwa kuku mmoja kwa mwaka.

Kwa bei ya 250 kwa yai.
💲Utapata 36,000 – 32,800 = 3,200 Tsh. Kwa iyo kwa kuku mmoja utavuna sh. 3200 k**a faida kwa mwaka.

ZINGATIA
👉Tumepiga hesabu kwa kuku mmoja, hivyo gharama zinakuwa kubwa kidogo ukilinganisha na uhalisia katika kuku wengi. Hata hivyo mambo mengine yamezitangatiwa.
👉Ingawa tumezingatia uhalisia hasa katika gharama, uwezekano wa faida kuongezeka kutoka 3200 hadi 5000 na zaidi kwa kuku upo mkubwa.
👉Kumbuka huu ni mwaka wa kwanza, kwa iyo faida imemezwa sana na kipindi acha utoto ambacho kuku alikuwa hazalishi kitu.

MWISHO
🐓Kwa kanuni (fomula) bora za vyakula, kwa bei nafuu wasiliana nasi.
🐓Ushauri kuhusu uendeshaji bora wa miradi ya ufugaji wasiliana nasi

Ufugaji Digital -MAPS
0755 639 835
0689 494 521 (watsapp)

23/05/2017

SEMINA ZA WAFUGAJI

Kutokana na uhitaji mkubwa wa maarifa na mbinu bora na zenye tija za ufugaji, TUMEJIPANGA kuwafikia wafugaji popote walipo! Lengo ni kutoa:

🐓MAFUNZO KWA VITENDO.
👉kutengeneza hyadroponics
👉kutengeneza mfumo na trei za hydroponics
👉formula za Vyakula bora kwa mifugo yote
👉kuotesha Azolla.

🐓Mbinu bora za ufugaji. (kuku, nguruwe, sungura, mbuzi, ng'ombe n. k)

🐓Masoko na mbinu za kuboresha bidhaa za mifugo
👉uchakataji wa bidhaa k**a maziwa, nyama n.k.

"Vikundi vya wafugaji" vyenye uhitaji, ama wafugaji binafsi wanaweza kujipanga na kujikusanya na kuwasiliana nasi kwa namba 0755639835, au 0689494521 (whatsapp).
Bei ni maelewano!!

UNAFUU WA MALISHO Hii ni picha tuliyotumiwa na mmoja wa wafugaji waliojifunza kwetu na kuchukua hatua. Ameahidi kupanua ...
16/05/2017

UNAFUU WA MALISHO
Hii ni picha tuliyotumiwa na mmoja wa wafugaji waliojifunza kwetu na kuchukua hatua. Ameahidi kupanua uzalishaji ili kuongeza tija!
Hii inaitwa Hydroponics!!
Like page ujifunze na wengine!!
Ufugaji Wa Kuku Kilimo Ufugaji

Kuandaa mtindi/ maziwa mala. Moja ya biashara inayorudisha mtaji haraka.
21/03/2017

Kuandaa mtindi/ maziwa mala.
Moja ya biashara inayorudisha mtaji haraka.

JE NI KWELI NGURUWE WANALIPA?Hesabu tunazokokotoa hapa chini zinazingatia vipimo vya uzalishaji na majedwali yaliyomo kw...
19/03/2017

JE NI KWELI NGURUWE WANALIPA?

Hesabu tunazokokotoa hapa chini zinazingatia vipimo vya uzalishaji na majedwali yaliyomo kwenye kitabu chetu!!

>Nguruwe mmoja toka anapozaliwa mpaka kufikia uzito wa kilo 90 atachukua siku 206 ambazo ni karibia miezi saba.

>katika siku hizo zote atakula kilo 292 za chakula ukizingatia mchanganuo katika jedwali namba 3 wa kulisha.

>Jedwali namba 2 la vyakula, mchanganyiko namba 3 unaghalimu takribani Tsh. 51000 kwa kilo 100. Inamaana kilo 1 ya chakula ni Tsh. 510. Kwa iyo kilo 292×510 = 148,920. Hii ni gharama ya kulisha nguruwe mmoja miezi 7.

>Matunzo na gharama nyingine zinakadiriwa kuwa Tsh. 200 kwa siku. Kwaiyo 200×206 (siku zote) = 41,200 Tsh.

>Gharama za kumtunza nguruwe mmoja, yaani chakula na matumizi mengine itakuwa: 148,920+41,200= 190,120 Tsh.

>Kwa nguruwe wa kilo 90 tumesema kitabuni kwamba utapata nyama asilimia 65 hadi 80 (umeshatupa uchafu wote yaani kicha, miguu, utumbo n.k.) tuchukue kiwango cha chini, hivyo; 65%×90kg= kilo 58.5 za nyama.

>Kilo ya nyama kadiria ni Tsh 5000. Hivyo 5000×58.5= 292,500 Tsh.

>Faida ni sawa na mapato toa matumizi: 292,500 - 190,120= 102,380 Tsh.

>Tumesema katika kitabu kwamba nguruwe 1 atakupa watoto 14 kwa mwaka makadirio ya chini kabisa (tumeshatoa idadi ya watoto wanaoweza kufa katika ukuaji)

>kwa iyo 14×102,380 =1,433,320 Tsh. Hii ni faida unayoipata kwa watoto wa nguruwe mzazi mmoja.

>Kumbuka hesabu hii inatoka kwa nguruwe mmoja, ukikokotoa kwa kundi la nguruwe unapata faida na “economies of scale” hivyo gharama zinaweza kupungua na faida kuongezeka.

>MUHIMU: Ni lazima utumie mchanganuo na vyakula tulivyoweka kwenye kitabu ili ufikie uzito huo kwa wakati tajwa.

Je ni kweli nguruwe wanalipa??
Kupata kitabu chetu, Tsh. 6000
0755 639 835

Karibuni tufuge kisasa
02/03/2017

Karibuni tufuge kisasa

Kitabu cha ufugaji bora wa nguruwe! Tayari kinasambazwa mikoani, wote walioweka oda watapokea ujumbe kitakapofika katika...
01/03/2017

Kitabu cha ufugaji bora wa nguruwe!
Tayari kinasambazwa mikoani, wote walioweka oda watapokea ujumbe kitakapofika katika maeneo yao.

Kwa maelezo zaidi 0755639835
UFUGAJI NI BIASHARA.

02/02/2017
CHAKULA CHA MIFUGO

Kuchanganya chakula cha mifugo vizuri ni msingi mkuu wa afya njema ya mifugo yako. Fanya hivi!

Unapochanganya chakula fanya hivi.

04/01/2017

KITABU CHA UFUGAJI WA NGURUWE

 Mwaka huu (2016) ulikuwa mwema sana. Tunashukuru kwa kutufanya kuwa Mwenza wako Mfugaji. Ni Furaha yetu kutoa mchango u...
31/12/2016


Mwaka huu (2016) ulikuwa mwema sana. Tunashukuru kwa kutufanya kuwa Mwenza wako Mfugaji. Ni Furaha yetu kutoa mchango uliokusogeza hatua kadhaa mbele.

Mwaka 2017 ni mwema zaidi. Mchango wetu kwako utaendelea kuwa dhahili zaidi. Tuingie na mtazamo chanya, hatuna migodi ya dhahabu ila TUNAYO MIFUGO.
Tujivunie ufugaji wetu, tuuboreshe, na tuweke ubunifu zaidi ili tuongeze tija.
UFUGAJI NI BIASHARA
TUNAMSHUKURU MUNGU

Ufugaji wenye nia, Ufugaji wenye kujali, Ufugaji wa mafanikio. Kuwekeza ni muhimu k**a tunahitaji matunda bora.  Tunampo...
25/12/2016

Ufugaji wenye nia, Ufugaji wenye kujali, Ufugaji wa mafanikio.
Kuwekeza ni muhimu k**a tunahitaji matunda bora. Tunampongeza dada kwa kuthubutu.

Nimejaribu kuotesha hydroponic foders. Leo ni Siku ya nne. Asante Ufugaji digital Kwa trays.

 Siku moja tukiwa tumemtembelea mfugaji, alikuwa na kuku 140 wa mayai. Alikiwa anakusanya wastani wa mayai 70 kwa siku k...
16/12/2016


Siku moja tukiwa tumemtembelea mfugaji, alikuwa na kuku 140 wa mayai. Alikiwa anakusanya wastani wa mayai 70 kwa siku kiwango ambacho ni kidogo mno kwa kuku aliokuwa nao na umri wao.

Tuligundua yalikuwepo matatizo mengi sana yaliyosababisha uzalishaji mbovu. Matatizo haya yalikuwa kwenye: ulishaji, banda, na usimamizi wa kila siku.

K**a kuku wako wanatoa mayai chini ya asilimia 80 uwe na uhakika kuna sehemu kuna shida.
Unahitaji huduma zetu.

Address

Nzasa
Dodoma
CHIHANGA,NZASA

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufugaji Digital -MAPS posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ufugaji Digital -MAPS:

Videos

Share

Category


Other Urban Farms in Dodoma

Show All

You may also like