Afya Za Wanyama Tanzania

Afya Za Wanyama Tanzania This page is allowing farmers to learning all about diseases and major controls straight forward to

we draft the business plan corncerning to veterinary services like starting farm and abottour

03/05/2023

UMO BATIKI
Habari mpya Kwa wafugaji ni kupendeza na batiki nzuri na bei nafuu
+255753709062
+255621059278

Haya Sasa wafugaji na wajasiriamali kazi kwenu...Tunakwambia mfugaji ni KUPENDEZA na UMO BATIKI!Hawa ni watengenezaji wa...
03/05/2023

Haya Sasa wafugaji na wajasiriamali kazi kwenu...
Tunakwambia mfugaji ni KUPENDEZA na UMO BATIKI!

Hawa ni watengenezaji wa batiki bomba kabisa zilizo na kiliwango Cha hali ya juu k**a unavyoona...

Wanapatikana Dar es salaam na Mikoani wanatuma Kwa UAMINIFU mkubwa.
Pia unaweza ukatoa oda na sample ya batiki au kikoi na wakakutengenezea Kwa haraka na Kwa bei nafuu sana!

Hebu wapigie na uwaulize chochote kuhusu batiki na vikoi nao watakujibu Kwa haraka na bashasha kwelikweli
+255753709062
+255621059278

Mfugaji tunakwambia hivi "Vaa, pendeza Kisha tukafuge!

04/04/2023

TATIZO LA HENIA KWA NG'OMBE
(Umbilical Hernia).

Henia hutokea Kwa wanyama wa aina mbalimbali ikiwemo ng'ombe, mbuzi na kondoo.

AINA ZA HENIA.
Kuna aina nyingi, ila hapa tumekuletea henia eneo la kitovu(umbilical hernia).

UTOKEAJI WAKE.
Henia husababishwa na mambo mengi yakiwemo kurithi, ugonjwa au kujeruhiwa na kitu cha ncha butu au kali.

KUDHIBITI.
Katika kudhiti, unaweza ukadhibiti henia itokanayo na kujeruhiwa, lakini hizo zingine inakuwa ngumu KUDHIBITI, Kwa mfano yakurithi.

TIBA
Hakuna tiba ya uhakika kutibu henia isipokuwa kupanya upasuaji(Surgery).

ZINGATIA.
Unapoona uvimbe wowote Kwa mnyama wako, epuka kutoboa, kuchoma Kwa kitu cha ncha Kali au namna yoyote itakayoleta athari Kwa mnyama. Toa taarifa kwa mtaalamu wa mifugo aliyekaribu nawe au wasiliana nasi kwa msaada zaidi.
+255784244081

01/01/2023

Kuanzia wiki hii tutaanza masomo mbali mbali ya magonjwa ya minyoo ya mbwa na paka.

ni kati ya ugongonjwa tutakaouchambua kiundani sana. Mbwa huyo anayeonekana kwenye picha ameathirika na ugongonjwa huo kwa kiasi kikubwa.

K**a utakuwa na maoni kuelekea mada za magonjwa yatokanayo na minyoo, tungependa tupate mawazo yako tafadhali kwa kuacha comment yako hapa au kujumbe mfupi kupitia namba 0784244081.

01/01/2023

Athari za minyoo kwa paka

01/01/2023

Tazama
Namna minyoo inavyoweza kuleta madhara kwa mbwa wako na huenda ikapelekea kifo

Afya Za Wanyama Tanzania tunawatakia wafugaji wetu wote heri ya mwaka mpya 2023.Tuanze mwaka tukiwa na nguvu mpya, hari ...
31/12/2022

Afya Za Wanyama Tanzania tunawatakia wafugaji wetu wote heri ya mwaka mpya 2023.

Tuanze mwaka tukiwa na nguvu mpya, hari mpya na matamanio mapya katika ufugaji wenye tija.

Pia tunakuomba wewe mfugaji wetu na mteja wetu unayefuatilia ukurasa huu utushauri juu ya makala au machapisho yetu tuongeze nini na tupunguze nini.

Unaweza tutumia ujumbe wako kwa njia ya ujumbe mfupi kwa namba 0784244081 au ukaweka comment yako hapa huku ukitaja mahali ulipo.

Ahsanteni!

11/08/2022

PARADUNDO YA KUKU.
(Avian Paratyphoid)

Kwa mara nyingi wafugaji na baadhi ya watu wamekuwa wakishindwa kutofautisha magonjwa.

Kuna huu ugonjwa unafahamika k**a TAIFODI(Typhoid) na huu unaojulikana kwa jina la PARATAIFODI(Paratyphoid). Haya ni magonjwa mawili tofauti lakini yanasababiswa na aina moja ya mazingira wakati bakteria anayeeneza magonjwa hayo pia ni tofauti, ambaye ni Salmonella paratyphi kwa ugonjwa wa paratyphoid na Salmonella typhi kwa ugonjwa wa typhoid.

SABABU YA UGONJWA.
Mara zote sababu za magonjwa ya tumbo kwa wanyama hutokana na uchafu pamoja na ungalizi mbaya.

Kinyesi, mabaki ya chakula na taka taka vinapoingia ndani ya maji wanayokunywa kuku, hupelekea chanzo cha ugonjwa huo wa paratyphoid.

UMRI ATHIRIKA.
Vifaranga wenye umri kuanzia wiki tatu na kuendelea, hawa ndiyo hushambuliwa na ugonjwa huo.

DALILI.Kuacha kulaKudhoofuKuharishaKinyesi kuganda kwenye njia ya hajaUkuaji hafifuKujisaidia damuWagonjwa huonekana k**a wanahisi baridi

KINGA.
Zingatia USAFI.
0784244081.

08/08/2022

Wafugaji na wakulima tunawatakia heri ya siku ya NANE NANE huku tukiwakumbusha kujiandaa KUHESABIWA katika zoezi la SENSA-2022.

Pia tunaomba radhi kwa kuchelewa kujibu comments zenu kwa wakati.

Hivyo, tunaomba mtume ujumbe au kupiga simu kwa namba iliyopo kwenye ukurasa ili kupata huduma kwa wakati!

Ahsanteni na endeleni kualika watu ku-like, ku-comment, ku-share na ku-follow.

02/08/2022

Sisi Afya Za Wanyama Tanzania tunatangazia wafugaji na watu wote kuwa tunasambaza vifara wa kuku aina ya kuroila kuanzia wenye siku sifuri(DOCs) na kuendelea kwa bei NDOGO sana!

0748169427
Tupigie muda wowote ili uletewe.

Pia na kuku wa kienyeji wanapatikana kwa oda MAALUMU.

Ukipata ujumbe huu, sambaza na umjulishe na mwingine!

01/08/2022

HOMA YA MIFUPA KWA KUKU.
(Avian Bone Fever).

Huu ni ugonjwa unaoenezwa na bakteria aina ya chlamydia psittaci ambaye hupenya hadi kwenye urojo wa mifupa(bone marrow).

Wanyama wanaoahirika zaidi na ugonjwa huu ni kuku, bata mzinga na bata maji ambao hufahamika k**a avian chlamidiosis.

Ukiacha wanyama hao, ndege aina ya KASUKU ndiye muathirika mkuu na hapo huitwa parrot fever.

Ugonjwa huu unaweza kuhama kutoka kwa ndege kwenda kwa binadamu(zoonotic disease)

SABABU ZA UGOJWA.
Katika sababu, tutaelezea chache.

Zifuatazo ni sababu kuu:-
1. Uchafu wa vyombo na banda
2. Idadi kubwa ya mifugo kwenye eneo dogo.
3. Kuchanganyika mgonjwa na wazima.

DALILI.
Wanyama walioathirika huonekana na:-
1. Kuvimba macho.
2. Kukatika sauti
3. Kukoroma na kushindwa kupumua.
4. Kulala kila wakati
5. Kukosa hamu ya kula
6. Manyoya kuvurugika
7. Kupungua uzito
8. Kutoa mharo wa kijani au njano kijani
9. Vifo

KINGA.
Ili kukinga, dumisha usafi.

TIBA.
Muite mtaalamu wa mifugo ili athibitishe na kushauri aina ya tiba.

0784244081

28/07/2022

Anza ufugaji wa sungura au samaki nasi tutakusaidia kufikia malengo yako kwa kukupatia vitabu vya miongozo kwa gharama nafuu Sana.

Ili kufuga sungura au samaki kwa tija, itakubidi upate mtaalamu. Sisi Afya Za Wanyama Tanzania tupo tayari kukusaidia kwa kila hatua popote ulipo ndani ya Tanzania au nje.

Tuna magrupu ya WhatsApp ambayo huwa tunafundisha mtu mmoja mmoja, vikundi au taasisi.

Ili kuwa mwanafamilia wa AFYA ZA WANYAMA CLUB Ni rahisi tu, tuma ujumbe wako kupitia namba iliyopo juu kwenye ukurasa huu na ujitambulishe mahali ulipo, jina, Aina ya mifugo uliyonayo na idadi yao.

Kwa wale watakaopenda kupata T-shirt zetu za Afya Za Wanyama Club, zipo na bei yake ni Tsh.20,000/- tu.

PUMU YA MBWA(Dog Asthma).Pumu ni ugonjwa unawakumba binadamu na wanyama pima.Huu Ni ugonjwa wa aleji(allergy) unaokwenda...
11/07/2022

PUMU YA MBWA
(Dog Asthma).

Pumu ni ugonjwa unawakumba binadamu na wanyama pima.Huu Ni ugonjwa wa aleji(allergy) unaokwenda kusumbua mifumo na njia za hewa kwa mnyama.

Kwa mbwa, pumu humpata katika umri wowote.

Sababu za pumu zipo nyingi lakini tutaelezea zile kuu ambazo huonekana kwa macho kabla ya vipimo vya ziada.

SABABU ZA PUMU KWA MBWA.
Sababu za pumu kwa mbwa zipo nyingi zikiwemo;
1. Vumbi la maua ya mimea(pollen).
2. Chakula chenye fangasi(mabaki ya chakula yaliyovunda).
3. Kuvuta sigara Kisha kukuhudumia mbwa au kumvutisha.
4. Vifaa vya usafi pia Ni sababu zitakazo pelekea pumu kwa mbwa. Vifaa hivi Ni K**a sabuni zenye marashi, kapeti linalonyofoka manyoya au sufi.

DALILI KUU.
1. Kuhema kwa kupumzika.
2. Kupumua haraka haraka.
3. Mapigo ya moyo kuwa juu hadi zaidi ya kawaida ambayo Ni 120/60 kwa dakika.
4. Kukohoa kwa kushtukiza.
5. Kupumua kwa shida.
6. Kuishiwa na nguvu.
7. Fizi kuwa na rangi ya buluu kutokana na kupungua kwa kiwango Cha oksijeni mwilini.
8. Kupoteza hamu ya kula na kuanza kudhoofu. Hatua hii huwa Ni ya mwisho na hapa kifo kinaweza kikatokea k**a hatowahiwa kupata tiba.

KUDHIBITI.
Ili kudhiti au kuepuka mbwa wake kupata pumu, inakubidi kuepuka sababu tajwa hapo juu.

TIBA.
K**a mbwa wake amekumbwa na na pumu na mtaalamu wa mifugo amethibitisha hilo, basi utatibu kwa kutumia vitamini D ukichanganya na homoni ya cortisone ili kupunguza uvimbe(inflammation) katika njia za hewa. Pia unaweza ukatumia Antihistamines ili kushusha kiwango Cha aleji mwilini.

USHAURI.
Unapoona dalili usizozifahamu kwa mbwa wake, toa taarifa kwa mtaalamu wa mifugo aliyekaribu yako au ofisi za mifugo zinazopatikana eneo ulipo.

Pia wawezawasiliana nasi kupia namba za simu zinazopatikana kwenye ukurasa huu au barua pepe [email protected] au acha ujumbe wako hapa nasi tutauona na tutakuhudumia haraka iwezekanavyo.

29/05/2022

Tupo kukuhudumia masaa 24Hrs popote ulipo.

Tupigie simu +255748169427

Zijue Bei za huduma zetu:-1. Chanjo ya kichaa Cha mbwa(Rabies) Tsh.20,000/=2. Kutembelewa Tsh. 15,000/=.3. Ushauri Tsh.5...
14/05/2022

Zijue Bei za huduma zetu:-
1. Chanjo ya kichaa Cha mbwa(Rabies) Tsh.20,000/=
2. Kutembelewa Tsh. 15,000/=.
3. Ushauri Tsh.5,000/=
4. Chanjo ya DHLP(Parvo) Tsh.35,000/=
5. Kupima mimba (PD) Tsh. 10,000/=
6. Fomula ya chakula Tsh.35,000/=
7. Chanjo ya CCPP Tsh.10,000/=
8. Chanjo ya CBPP Tsh.10,000/=
9. Chanjo ya minyoo Tsh.10,000/=
10. Kusafiri na mtaalam Tsh.50,000/= kwa siku.

NB: Bei za matibabu zitategemea ugonjwa na urefu wa dozi.
0748169427.

14/05/2022

Je, ungepebda kufunga mitambo mikubwa au machine ya aina yoyote na bado hujapata jibu?

Sasa Afya Za Wanyama Tanzania tumekusikia. Tumeamua kuanzisha idara ya ufundi wa umeme wa Viwandani, ambapo tuna mafundi wabobezi na wenye weledi wa kazi za umeme mkubwa.

Hivyo ukihitaji kufundua kiwanda Cha kutengeneza vyakula vya mifugo tutakupa wataalam watakaokushauri pia juu ya ukubwa wa mota na saizi ya kinu.

Pia kwa ushauri tupigie muda wowote tutakushauri kupitia idara husika
0748169427

15/04/2022

Afya Za Wanyama Tanzania inapenda kuwatangazia mfumo mpya wa kupata huduma zetu kwa kutumia kadi maalumu.

Mfumo huo unaoitwa WANYAMA PREPAID CARD utakuwezesha kupata huduma za matibabu, ushauri, chanjo na kutembelewa shambani pale tu unapokuwa na kadi hiyo.

Ghaeama ya kadi ni Tsh. 33,400/- kwa mwezi ambapo utaweza kupata huduma zote Mara mbili kwa mwezi.

Kwa maelezo zaidi tupigie kupitia namba zetu
+255712189941
+255748169427


Twen'zetu shambani..

21/02/2022

Weka maoni yako kulingana na huduma zetu ili tuziboreshe zaidi

15/02/2022

Kumekuchaa..

Wakazi wa Chanika na Pugu kajiungeni, tunawaletea semina ya ufugaji wa kuku kibiashara!

SIKU: MARCH,2022
UKUMBI: CHECK POINT
MUDA: 4Asbh-7Mchana
MADA: MAGONJWA YA KUKU NA TIBA ZAKE, LISHE BORA YA KUKU NA UANDAAJI WAKE.
SIMU: +255 748 169 427.

Kuhusu tarehe, itatajwa.

K**a utapenda kushiriki, tupigie simu au meseji ili tuandae siti yako.

Wataalamu wa mada zote tajwa hapo juu watakuwepo kukulisha madini!

Semina hii ni BUREEE..!

Usipange kukosa!
0748169427


Njoo tufuge..




12/02/2022

Ukiwa k**a mfuatiliaji wetu wa ukurusa wa Afya Za Wanyama Tanzania, je tumeweza kukusaidia kwa kiasi gani kufiki malengo yako katika ufugaji wako?

Mrejesho wako ni wa muhimu kwetu ili tuufanyie kazi!

03/02/2022

Karibu tupokee oda yako ya vifaranga bora wa kuroila kwa bei ya Tsh.1,520/-@.

Tunapatikana Dar Es Salaam.
Mikoani tunatuma kwa usalama wa hali ya juu!

Mawasiliano:
+255(0)748169427

29/01/2022

Je, unapenda kufuga lakini hujujui wanyama wa mbegu bora utapata wapi?

Usiwaze..!
Tupigie ili tukuhudumie kwa kukupatia mifugo bora 0712 189 941.

Utapata:-
`kuku aina zote
`ng'ombe aina zote
`sungura aina zote
`mbwa aina zote.
`bata na kanga.

Tupigie: 0712 189 941

Address

Kibwegere
Dar Es Salaam
UBUNGO

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Telephone

+255784244081

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Za Wanyama Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Afya Za Wanyama Tanzania:

Videos

Share

Category


Other Veterinarians in Dar es Salaam

Show All

You may also like