19/04/2022
MAKOSA MATANO WANAYOFANYA WAFUGAJI.
Wafugaji wengi huwa na kasumba au matatizo mengi katika kuendesha biashara zao za ufugaji ikiwemo na:
1. Kujua undani wa mbegu anayoingiza shambani kwake.
Hili ni tatizo linalosumbua wafugaji wengi na kwa muda mrefu sasa, yaani mfugaji akisikia kuna mtu anauza KUCHI na yeye atataka bila kujua ni mbegu gani ya kuchi, ubora wao upoje na udhaifu wao upoje ila kwa kuwa kaambiwa kuchi wanalipa utakuta anakimbizana kuingiza hiyo mbegu shambani bila kukusanya taarifa sahihi kwa lengo la kuokoa mtaji wake na malengo yake.
2. Kutokuwa na mtaalamu wa kuaminika.
Wafugaji wengi hawana wataalamu wa uhakika yaani huwa na madaktari wengi kiasi kwamba ikitokea mifugo yake inaumwa huwa anachanganya madawa hadi mfugo unachanganyikiwa.
3. Malengo makubwa ya ufugaji wake.
Wafugaji wengi huwa hawana malengo endelevu ya ufugaji hali hii huwafanya wawe ni watu wasio na misimamo ya bei na ubora unaoeleweka.
Ni miaka sasa kuku wa nyama wanauzwa 5000+ na hata k**a vifaranga vitauzwa bei basi ukosefu wa misimamo hujikuta wajasiriamali wengi wafugao kuku huishia kulalamika na sio kusimamia wanachokiamini.
4. Elimu ya ujasiriamali na uwekezaji
Ni tatizo linalowafanya wafugaji wabaki palepale licha ya kuwa na mitaji ila ukosefu wa elimu umesababisha mitaji kufa na masoko kudumaa miaka yote.
5. Muendelezo
Ni hatua ya kuendeleza kile ulichokianza, hii imesababishwa na tabia ya mazoea iliyopelekea wateja hao wakose biashara endelevu.
baadaye